KANUNI ZA KUTEMBEA NA ROHO MTAKATIFU NA NGUVU ZAKE-01

“Nanyi MTAPOKEA NGUVU AKISHAWAJILIA JUU YENU ROHO MTAKATIFU…”

MDO 1:8

1. Hii nguvu HAIJITEGEMEI inaambatana na UWEPO WA ROHO MTAKATIFU, ukiondoa uwepo wa Roho mtakatifu na NGUVU SAHAU, INAONDOKA (Matendo 10:38).

VITU VINAVYOONDOA UWEPO WA ROHO MTAKATIFU;

A). DHAMBI, HASA DHAMBI ZA SIRINI AMBAZO WENGINE HAWAKUDHANII KUWA UNAWEZA KUWA UNAZITENDA, YAANI ZILE AMBAZO ZIKIWEKWA WAZI, WATU WANAPIGWA NA BUTWAA AU KUSEMA KAMA NA DCK NAYE YUKO HIVI, BASI HALI NI MBAYA.

Isaya 59:1-2

Zaburi 66:1

B). KUTOTII SAUTI YA ROHO MTAKATIFU NA MISUKUMO YA ROHO MTAKATIFU (TO DISOBEY THE VOICE AND THE PROMPTS OF THE HOLY SPIRIT)

Hapa namaanisha mfano umekaa sehemu halafu ghafla, UNASIKIA NDANI YA KUWA “ACHA HAWA WAGENI HAPO SEBULENI, NENDA NDANI KAOMBE” halafu wewe unajifanya mstaarabu namba moja duniani na kusema, “NITAOMBA HATA BAADAE” nakuhakikishia, UNAUA USHIRIKA NA URAFIKI WAKO NA ROHO MTAKATIFU, UKIENDELEA HIVI, ITAFIKIA MUDA ATAUCHUNA KIMYA (ATAZIMA)!

Au mfano unamsikia MOYONI ANAKUKATAZA KUTAZAMA VIPINDI FULANI VYA TV, REDIO, MOVIE, ANAKUAMBIA FUTA HIYO INSTAGRAM YAKO HAINA FAIDA INAKULA KIROHO CHAKO NA KUKUCHOCHEA KUWAZA MABAYA NA KUTENDA VIBAYA au ANAKUAMBIA KUANZIA LEO, ANZA ZOEZI LA KUWEKA SIMU PEMBENI WALAU MASAA 3 BILA SIMU, ILI USIWE MTUMWA WA HIYO SMARTPHONE, LAKINI WEWE UNAJIFANYA MJUAJI!

Mfano anakuambia, USIENDE KUANGALIA MECHI YA MPIRA, HUO MUDA UTUMIE KUSOMA NENO NA KUOMBA, UTATAZAMA MATOKEO BAADA YA MECHI MAANA KUANGALIA AU KUTOKUANGALIA HAKUTABADILI MATOKEO YALIYOPASWA KUTOKEA, LAKINI WEWE UNAJIFANYA KICHWA NGUMU NA KUTAZAMA MECHI BADALA YA KUKAA NAYE FARAGHA, ATAKUNYAMAZIA, NA UTAANZA KUPOA NA KUFA KIROHO!

HIKI NI KITU AMBACHO WENGI NI UHALISIA AMBAO UNAWATOKEA NA WENGI MMEANGUKA KWENYE DHAMBI NA ADDICTION KIBAO KWA SABABU YA KUTOITIKIA NA KUTII MISUKUMO YA ROHO MTAKATIFU!

C). KUTOMJENGEA MAZINGIRA YA IBADA

“…Nao walipokuwa WAKIMFANYIA MUNGU IBADA NA KUFUNGA, ROHO MTAKATIFU AKASEMA…”

(MDO 13:2).

-Roho MTAKATIFU anasema sana kwenye mazingira ya IBADA NA MIFUNGO.

•Kuwa mtu wa sifa

•Kuwa mtu wa shukurani na si lawama

•Usisubiri utendewe muujiza ndipo ushukuru au kusifu, fanya hata katikati ya vita (Mdo 16:24-25).

•Usisubiri usukumwe na Roho Mtakatifu kufunga, JIWEKEE RATIBA YAKO YA KUELEWEKA KILA WIKI YA KUFUNGA na hizo ambazo atakusukuma Yeye kufunga zitakuja zenyewe, but be A FASTING MACHINE!

NARUDIA, YEYE HUPENDA MAZINGIRA YA IBADA NA MIFUNGO, MTENGENEZEE MAHALI PA IBADA NA MIFUNGO NAYE ATAKAA HAPO (Kutoka 25:8)!

TENDEA KAZI HAYA KWANZA,

MENGINE YATAKUJA WAKATI MWINGINE!

USIPENDE NOTISI, PENDA KUJIREKEBISHA PALE AMBAPO UMEONA KABISA UNAHARIBU, USIISHIE KUSEMA “MUNGU ATUSAIDIE” KUPATA TU HUU UJUMBE TAYARI MUNGU KAKUSAIDIA!

Mwalimu Dickson Cornel Kabigumila

14/05/2019

Mafundisho
yesunibwana

SIFA ZA MME BORA

  1. Yeye mwenyewe AMEMPOKEA YESU, NA KUJITIA CHINI YA MAMLAKA YAKE KAMA BWANA NA MWOKOZI WAKE KIBINAFSI (Yohana 1:12-13, Yohana 3:16-18). -Atambue thamani ya

Read More »

NDOA

Haikuanzishwa Na WANADAMU Bali MUNGU Ndiye Aliyeanzisha TAASISI HII… Imeanzishwa Na MUNGU Ambaye Ni Roho, Uwe Na Uhakika Haiwezi Kuendeshwa Kwa Kutegemea AKILI, HEKIMA NA

Read More »

HEKIMA ZA NDOA 3

  “Kusudi la ndoa ni kujenga TIMU YA WANAOSADIANA NA KUINUANA. Wawili ni bora kuliko mmoja, MAANA MMOJA AKIANGUKA, MWENZIE ATAMUINUA. Ndoa sahihi ni muunganiko

Read More »