HEKIMA KWA AJILI YA FEDHA

1. HAUWEZI KUWA NA FEDHA ZAIDI YA KIWANGO CHAKO CHA KUGUSA MAISHA YA WENGINE.
LUKA 6:38

“Kila mtu aliyeokoka au mpagani, ana kiwango cha pesa sawasawa na namna bidhaa, huduma au ujuzi wake UNAVYOGUSA NA KUHITAJIWA NA WATU WENGI WALIO TAYARI KULIPA AU KUTOA KWA AJILI YA WANACHOPOKEA KWAKE! Kama UNAGUSA WATU WACHACHE, UTAKUWA NA FEDHA KIDOGO, NA KAMA UNAGUSA MAISHA YA WENGI, UTAKUWA NA FEDHA NYINGI! Usikimbize pesa, ONGEZA MGUSO WAKO KWA WATU NAO WATAKUPA FEDHA UNAYOITAKA”

 

2. HUWEZI KUPEWA FEDHA NA WATU BILA KUWA NA KITU KILICHOWAGUSA TOKA KWAKO
ZABURI 45:12

“Hakuna mtu atakayekupatia PESA bila wewe KUGUSA MAISHA YAKE au KUKATA KIU YAKE FULANI! Inaweza kuwa kupitia BIDHAA BORA au HUDUMA NZURI UNAYOTOA, halafu WANAZAMA MFUKONI KULIPIA AU KUTOA KWA HIARI! Andiko hilo hapo juu linatuonesha BINTI TIRO ALILETA KIPAWA CHAKE KWANZA halafu MATAJIRI NDIPO WAKAJIPENDEKEZA KWAKE! Hakuna atakayejipendekeza kukupa PESA mpaka kuna KITU ANAFAIDIKA NACHO TOKA KWAKO”

 

3. HUWEZI KUPATA FEDHA ZAIDI YA THAMANI ULIYONAYO
LUKA 15:16

“Mwana mpotevu ALIPOFIKIA HATUA YA KUONA YEYE NI SAWA NA NGURUWE NA ANAWEZA HATA KULA MAGANDA WALIYOKUWA WAKILA maandiko yanasema WALA HAKUNA MTU ALIYEMPA KITU! Ikiwa na maana kwenye ulimwengu wa FEDHA watu HUWEKA PESA YAO KWA MTU AMBAYE ANA THAMANI/ ANA KITU NA SI VINGINEVYO! Ndio maana BWANA YESU alisema, ALIYE NACHO ATAONGEZEWA NA ASIYE KUWA NACHO HATA KIDOGO ALICHONACHO ATANYANG’ANYWA!”

 

4. HAUTAPATA PESA ZAIDI YA UWEZO ULIONAO
Mathayo 25:14

“Katika MFANO WA TALANTA, tunaona KILA MMOJA ALIPATA IDADI YA TALANTA si kwa kutegemea kiwango cha kujuana, elimu au uzuri wa sura bali SAWASAWA NA UWEZO WA KILA MMOJA! Mwenye UWEZO MKUBWA alipata FEDHA NYINGI kuliko WENZAKE wenye UWEZO MDOGO! Hii ni KANUNI INAYOTAWALA ULIMWENGU WA FEDHA! HAUWEZI KUPEWA au KULIPWA FEDHA ZAIDI YA UWEZO ULIONAO!”

 

5. FEDHA KAMA ILIVYO KWA VITU VYOTE VYA THAMANI, HAIKAI MAHALI PENYE USALAMA, HUKAA MAHALI PAGUMU NA PA HATARI KUIFIKIA, HIVYO INAHITAJI KUJILIPUA KUIPATA (2WAFALME 7:3-8)

“Ukishapata PICHA YA NINI UFANYE KIKUPE PESA, hiyo picha tu ndiyo inayopaswa KUKUPA NGUVU NA UJASIRI WA KUKABILI VITA, UPINZANI NA UGUMU NJIANI, maana KAMA UMEWEZA KUONA UWEZEKANO HUO, HESABU ZINAKUBALI UKIWA HAPO ULIPO, ni uhakika HIYO BIASHARA AU HUDUMA inaweza KUKULIPA. Hivyo UNAPASWA KUBAKI NA PICHA HIYO na KUVUKA KIKWAZO KIMOJA KIMOJA kama HAWA WAKOMA mpaka UMEISHIKA FAIDA MKONONI”

 

6.HUWEZI KUWA NA FEDHA ZAIDI YA UBORA WA KIAKILI ULIONAO
(1Samweli 18:5)

“Tunamuona Daudi hapo ANALAMBA PROMOTION mbele ya WAFANYAKAZI WENGI WAZOEFU ALIOWAKUTA kwenye JESHI LA SAULI, na bila shaka KAMA WALIKUWA WANALIPWA MISHAHARA basi HATA KIASI CHAKE CHA MSHAHARA KILIPANDA! Lakini SIRI PEKEE iliyompandisha Daudi ilikuwa KUTENDA KWA AKILI KATIKA KILA ALILOTUMWA! Unajua UBORA WA KIAKILI KWENYE KITU UNACHOFANYA utaamua UBORA WA BIDHAA AU HUDUMA, na matokeo yatakuwa FEDHA ZAIDI! Bila MATUMIZI YA AKILI YA KURIDHISHA, SAHAU KUWA NA PESA YA KUTOSHA”

Mafundisho
yesunibwana

WAZEE WA MKEKA/KUBETI MPOO!!

  USHUHUDA: AFUNGULIWA TOKA TABIA SUGU YA KUCHEZA KAMARI, MAARUFU KAMA KU-BET AU KUTANDIKA MIKEKA! Ngoja nikupe mchongo wa kukutoa jumla kwenye huu MSALA. Huu

Read More »
Mafundisho
yesunibwana

SEX BEFORE MARRIAGE

#TENDO LA NDOA KABLA YA #NDOA Luka 16:10 [10]Aliye mwaminifu katika lililo dogo sana, huwa mwaminifu katika lililo kubwa pia; na aliye dhalimu katika lililo

Read More »
Mafundisho
yesunibwana

KWA WAOLEWAJI TU

“Kati Ya Mambo Unayopaswa Kuyachunguza Kuhusu Mtu Anayetarajia Kukuoa NI UAMINIFU NA UADILIFU Kwenye MALI NA PESA YA UMMA, KAMPUNI Au WATU WENGINE… Ukiona Huyu

Read More »

NDOA

“Haiunganishi familia mbili bali inazalisha familia mpya ya tatu… Inayojiendesha, kujitawala, kujiamulia na kujichagulia mambo yake… Familia hii mpya ya tatu inakuwa na kusudi na

Read More »
ABC Global Radio
ABC Global Radio
LIVE