BABA WA KIROHO

(MASWALI NA MAJIBU)

Na, Mwalimu Dickson Cornel Kabigumila

1. Je utampataje na kumjua baba yako wa kiroho?

Jibu: NI KWA KUANGALIA MAMBO YOTE MATANO NILIYOSEMA KWENYE POST ZILIZOPITA KABLA YA HII;

i) Awe mtu wa rohoni na si mtu wa mwilini

ii) Kiroho chake kiwe juu ya chako

iii) Character yake (tabia, mwenendo na maadili) yasiwe na maswali.

iv) Awe mtu aliye na vitu ulivyobeba au aliyeweza kulea watu wenye vitu vya aina yako.

v)Awe mtu ambaye anaruhusu watu wamfuate kama yeye anavyomfuata Kristo, wakiona anapotea wamuache wabaki na Yesu!

NB: MSHIRIKISHE MUNGU KWA MAOMBI, MPAKA UWE NA AMANI NA UHAKIKA KABLA YA KUMFUATA MTU KUMUOMBA AWE BABA YAKO WA KIROHO.

BABA WA KIROHO

(Maswali na majibu)

2. Nani anamfuata mwenzake kujitambulisha, baba au mtoto?

Jibu: YEYOTE KATI YAO ANAWEZA.

-Eliya alimfuata Elisha,

-Yesu aliwafuata Zakayo, Mathayo, Petro na wengine wengi ambao walimfuata baada ya yeye kuwaambia NIFUATE!

-Wanafunzi wa Yohana walimfuata Yesu, wakaenda kwake na hawa kurudi tena kwa Yohana. Bali walianza kuwaleta wenzao kwa baba yao mpya, Yesu!

HIVYO, KUNA WAKATI BABA HUMFUATA MTOTO NA KUNA WAKATI MTOTO HUMFUATA BABA!

NAKUSHAURI UMFUATE BABA, USISUBIRI AKUFUATE!

BABA WA KIROHO

(Maswali na majibu)

3. Je ni lazima baba wa kiroho awe mchungaji au anachunga kanisa?

Jibu: HAPANA

Yesu hakuwa na jengo wala dhehebu analolichunga lakini alikuwa na watoto wa kiroho anaowalea na kuwaandaa!

Musa hakuwa na jengo na dhehebu lakini aliwalea akina Joshua na Kalebu na wale 70 waliokuwa chini yake.

MIMI NIMEANZA KULEA WANANGU WA KIROHO HATA KABLA SIJAWA MCHUNGAJI NA MWANZILISHI WA ABC!

UBABA NI MAJUKUMU, SI CHEO.

UBABA SI HUDUMA BALI NI UWAJIBIKAJI.

Nikiwa Mwalimu wa Neno la Mungu, tayari nilikuwa na watoto wa kiroho zaidi ya 70, niliokuwa nafuatilia maendeleo yao ya kiroho, uchumi, mahusiano, familia na malezi, makusudi waliyobeba, maono, ndoto na malengo yao, na kuwa simamia, kuwakazania, na kuhakikisha wanayafikia na kuyaishi!

Mtu yeyote aliye na sifa za ubaba, nilizotaja kwenye post zilizotangulia, na ANAWAJIBIKA, hata kama hachungi, huyo ni baba sahihi, kaa naye

BABA WA KIROHO

(Maswali na majibu)

4. Je ninaweza kubadili baba wa kiroho? Kama ndiyo, kwa sababu zipi?

Jibu: NDIYO, UNAWEZA KUBADILI BABA WA KIROHO.

Sababu za kubadili baba wa kiroho;

1. Ukigundua hana ulivyo navyo au hawezi kuvilea ulivyobeba, na hajawahi kulea mtu au watu wa aina yako!

Kwa Usalama wako, tafuta unakofit vizuri.

2. Akiwa na matatizo ya kitabia, maadili na mwenendo (character)!

Mfano ameshindwa kukaa kwenye ndoa yake, ameiacha imani, amejiunga na imani potofu, ameacha kumfuata Yesu, ameanza kuibia na kutapeli watu kwa jina la Yesu, ameanza masuala machafu kama uzinzi na zinaa, na mengine ya namna hii!

3. Pale unapokuwa na Yohana Mbatizaji, kumbe uliwekwa kwake kwa muda, akulee ila akija Yesu, ndiye haswa unayepaswa kuambatana naye!

Rejea: Habari za wanafunzi wa Yohana waliomuacha na kumfuata Yesu na kuwa wanafunzi wake (Yohana 1)!

NB: UKIFANYA BIASHARA YA KUHAMA HAMA KUTOKA BABA HUYU HADI YULE NJE YA SIFA HIZI, WEWE UNAKUWA NA MATATIZO, NA HUJUI HATA MAANA YA UBABA WA KIROHO.

BABA WA KIROHO

(Maswali na majibu)

5. Nini ni majukumu ya baba wa kiroho?

Jibu: MAJUKUMU YA BABA WA KIROHO;

i) Kuongoza kwa mfano (leading by doing), baba yeyote lazima awe kioo na walioko nyuma yake wajifunze kwake kwa matendo na si notice!

ii) Awe kioo cha kitabia (character image) kwa watoto wake.

iii) Awe mtu anayewaunganisha watu na Bwana Yesu na si kuchukua utukufu na mahali pa Yesu!

iv) Awe mshauri anayefuata baada ya Roho Mtakatifu kwa watoto wake.

v) Kuwatambulisha wanawe kwa walimu bora na makini waliomo ndani ya Kristo, badala ya kuwaaminisha kwamba yeye pekee ndiye ana kitu cha kuwafaa.

vi) Usimamizi na uangalizi (overseer and supervisor): Lazima awe msimamizi na mwangalizi wa vipawa, huduma, karama, wito na makusudi waliyobeba watoto wake!

Lakini pia lazima awe msimamizi wa hali zao kiuchumi, ndoa, familia, malezi nakadhalika!

BABA WA KIROHO

(Maswali na majibu)

6. Je naweza kuwa na baba wa kiroho zaidi ya mmoja?

Jibu: HAPANA HAIWEZEKANI, BABA NI MMOJA TU, ILA RUKSA KUWA NA WALIMU MAELFU MAELFU WA KUJIFUNZA KWAO ILA WALIO NA CHARACTER NA USHUHUDA WA KRISTO!

“Kwa kuwa ijapokuwa MNA WAALIMU KUMI ELFU KATIKA KRISTO, walakini HAMNA BABA WENGI. MAANA MIMI NDIMI NILIYEWAZAA KATIKA KRISTO YESU KWA NJIA YA INJILI. BASI NAWASIHI MNIFUATE MIMI…”

(1Wakorintho 4:15-16).

NAAMINI UTAPATA CHA KUKUSKUKUSAIDIA,

NI POST YA MWAKA 2017, IMERUDISHWA HEWANI LEO NA:

#RGG_Church

Aposto Astton Rgg

10Th MAY 2019

Mafundisho
yesunibwana

KWA WAOLEWAJI TU

“Kati Ya Mambo Unayopaswa Kuyachunguza Kuhusu Mtu Anayetarajia Kukuoa NI UAMINIFU NA UADILIFU Kwenye MALI NA PESA YA UMMA, KAMPUNI Au WATU WENGINE… Ukiona Huyu

Read More »

HEKIMA ZA NDOA 5

“Ni mwanandoa mpumbavu pekee anayesubiri aombwe msamaha ili asamehe; Maana waweza kukuta kile unachoona kama kosa, mwenzako anaweza asikione hivyo, kwa kutosamehe ufa huo unaweza

Read More »

NDOA

Haikuanzishwa Na WANADAMU Bali MUNGU Ndiye Aliyeanzisha TAASISI HII… Imeanzishwa Na MUNGU Ambaye Ni Roho, Uwe Na Uhakika Haiwezi Kuendeshwa Kwa Kutegemea AKILI, HEKIMA NA

Read More »