ATHARI YA MUZIKI KWENYE MAISHA YA MTU.

Kuna Aina mbili ya muziki, muziki wa kidunia na Muziki wa ufalme wa Mungu.

1 Samweli 16:23

[23]Ikawa, ile roho mbaya kutoka kwa Mungu ilipomjilia Sauli, ndipo Daudi akakishika kinubi, akakipiga kwa mkono wake, naye Sauli akaburudishwa, na ile roho mbaya ikamwacha.

Kila Muziki unaousikia masikioni mwako una nguvu nyuma yake na unazalisha aina ya Hisia ambazo au zitakusukuma ufanye jambo jema au ufanye dhambi.

Kila Muziki unasukumwa na tabia na roho inayofanya kazi kwa aliyeimba na waliopiga.

Muziki sio kitu cha kawaida kusema nasikia tu Bongoflavor kwani ni dhambi ! ( Shida sio kwamba kusikia muziki wa Bongoflavor ni dhambi, bali kutakufanya uwe mshiriki muda si mrefu, muziki una nguvu )

TUANGALIE SCENARIO YA SAULI NA DAUDI

Sauli anaingiwa na Pepo na linaanza kumsumbua na kumtesa

Daudi mwenye upako anapiga kinubi kwa ustadi na ghafla ile roho mbaya ndani ya Sauli inatoweka na Sauli anakuwa huru.

Maana yake kuna aina ya Muziki na upigaji ukiambatana na Roho inayofanya kazi kwa mwimbaji au mpigaji unaweza kutoa Pepo ndani ya Mtu na akawa huru

Vivyo hivyo kuna aina ya muziki na upigaji ambao unaweza kuingiza pepo ndani ya Mtu.

USICHUKULIE MUZIKI KAMA SEHEMU YA PLEASURE

elewa unaweza kuingiwa na mapepo kwa kuangalia Muziki.

Nitarudia Tena

Muziki ni nguvu inayoweza kuharibu maisha ya mtu na hisia zake na kusababisha tamaa na mwisho dhambi na uharibifu.

Kwa mfano

Unasikia Muziki wa Bongoflavor

Anayeimba anacheza na wadada wako Uchi na anawashikashika na biti na upigaji lazima uendane na step za kucheza na hisia za mwimbaji ( Nakuhakikishia kuna roho za giza zinaingia kwenye maisha yako )

USICHUKULIE KUSIKILIZA MIZIKI YA BONGOFLAVOR KAMA KITU CHA KAWAIDA

wewe angalia mpaka hapo kama hisia zako na maisha yako yana usalama .

Angalia kwa umakini

“ Usisikie kila wimbo na kila muziki, angalia miziki yenye nguvu za Mungu za kuponya Hisia zako na maisha yako ”

Isaya 55:3

[3]Tegeni masikio yenu, na kunijia;

Sikieni, na nafsi zenu zitaishi;

Kuna uzima kwenye kusikia

Lakini pia kuna kifo kwenye kusikia.

Chukua hatua na

Maisha yako yatakuwa salama

Pastor Ibrahim Amasi

ABC-KAHAMA

LivingWord

@2019

Mafundisho
yesunibwana

KWA WAOLEWAJI TU

“Kati Ya Mambo Unayopaswa Kuyachunguza Kuhusu Mtu Anayetarajia Kukuoa NI UAMINIFU NA UADILIFU Kwenye MALI NA PESA YA UMMA, KAMPUNI Au WATU WENGINE… Ukiona Huyu

Read More »

NDOA

Haikuanzishwa Na WANADAMU Bali MUNGU Ndiye Aliyeanzisha TAASISI HII… Imeanzishwa Na MUNGU Ambaye Ni Roho, Uwe Na Uhakika Haiwezi Kuendeshwa Kwa Kutegemea AKILI, HEKIMA NA

Read More »

NDOA

“Haiunganishi familia mbili bali inazalisha familia mpya ya tatu… Inayojiendesha, kujitawala, kujiamulia na kujichagulia mambo yake… Familia hii mpya ya tatu inakuwa na kusudi na

Read More »