NGUVU ATOAZO MUNGU ZA KUPATA UTAJIRI

“Bali Utamkumbuka BWANA, Mungu Wako, MAANA NDIYE AKUPAYE NGUVU ZA KUPATA UTAJIRI…” (Kumbukumbu 8:18).

Hapa Tumesoma Ya Kuwa Mungu Anatoa NGUVU ZA KUPATA UTAJIRI, Na Haisemi Mungu Anatoa UTAJIRI!

Mungu Anakupa Wewe NGUVU Itakayokusaidia (KAMA UTAITUMIA) Ili Ikusaidie UUPATE UTAJIRI.
Kwa Lugha Nyepesi, Unaweza Kuwa Na Nguvu Hizi Tatu, Lakini Usipoziweka Kwenye UTENDAJI, Ukakaa Tu, UTAKUFA NA UMASIKINI WAKO!
Yeye Mungu Anakupa NGUVU ZA KUPATA UTAJIRI; Wewe Ndiwe Unayechukua Hatua Ya “KUUTAFUTA UTAJIRI” Maana Hizo Nguvu Zinakusaidia Wewe “KUUPATA UTAJIRI”

Nguvu Anazotoa Mungu Kwa Mtu Ili Aweze Kuupata Utajiri Ni Hizi Hapa Tatu;

1.NGUVU ZA KIROHO/ NGUVU ZA ROHONI

Kwakweli, Kila Kitu Unachokitaka Kwenye Maisha Haya Ya Hapa Duniani Kina Msingi Na Asili Au Mwanzo Kwenye Ulimwengu Wa Roho/ Rohoni.
Na Ulimwengu Wa Roho Una Serikali Kuu Mbili; Serikali Ya Mungu Aliye Hai, Na Serikali Ya Ibilisi, Shetani.

Hizi Serikali Mbili Ndizo Zinazoamua Mafanikio Au Kushindwa Kwa Mwanadamu Huku Duniani.
Na Hakuna Mwanadamu Ambaye YUKO SEHEMU ZOTE MBILI; Ni Aidha Uko Kwa Mungu Ama Kwa Ibilisi.

Ukiwa Kwa Ibilisi Kupitia Mfumo Wako Ulio Kinyume Na Mapenzi Ya Mungu Na Maagizo Ya Neno Lake, Kufanikiwa Kwako Kutategemea KUVUNJA SHERIA, WIZI, RUSHWA NA KUKWEPA HAKI!
Ukiwa Kwenye Serikali Ya Mungu Ili Ufanikiwe Ni Lazima Uzingatie SHERIA, UWE MWAMINIFU, MWENYE HAKI NA UKWEPE NJIA ZOTE ZISIZO HALALI KWA MUNGU NA WANADAMU!

Ukimtii Mungu Na Kuvumilia Kudumu Katika Kutenda Yake, Baada Ya MUDA Utachomoza Na Kuanza Kwenda Mahali, NURU YAKO ITATOKEA MARA Kama MATOKEO YA UTIIFU WAKO KWA MUNGU.
Ukiwa Upande Wa Ibilisi, Kufanikiwa Kwako Na Kustawi Kunategemea Kudumu Katika Kutenda Uovu Na Kuvunja Taratibu Halali Za Mungu Na Wanadamu. Na Utafanikiwa Na Kuchomoza HARAKAHARAKA Lakini ANGUKO LAKE PIA NI KUBWA NA LA GHAFLA; UTATOWEKA KAMA MOSHI, UTATOWEKA KAMA UMANDE WA ASUBUHI, Mafanikio Na Utajiri Wako Unakuwa Wa Muda, Na Unaiangamiza Roho Yako Kama HAUTAGHAIRI NA KUMREJEA MUNGU MAPEMA!
Wanaodumu Na Mungu, Na Kukubali KUSOTA KWA HAKI NA UAMINIFU, Hawa HUKUSANYA TARATIBU Lakini UTAJIRI NA HESHIMA YAO HUDUMU; Maana Kuna Nguvu Ya Mungu Nyuma Kulinda Kila Walichonacho Na Wakipatacho!
HII NDIYO NGUVU YA KIROHO AITOAYO MUNGU; INAYOKUSAIDIA UFANIKIWE NA KUMZUIA YULE ALAYE!

Baadhi Ya Mambo Ya Kufanya Ili Uwe Na Nguvu Za Kiroho Kwenye Eneo La MAFANIKIO NA UTAJIRI; Uwe Mwaminifu Kwenye Fungu La Kumi Na Sadaka Za Kawaida (Malaki 3:8-11), Wahurumie Na Kuwasaidia Masikini, Wahitaji; WAJANE, YATIMA, WAGONJWA, WAFUNGWA (Mithali 19:17), Jizoeze Kuwa MTOAJI Kwa Watu Wengine Kwanza Kama Unataka Watu Wakupe Vitu (Luka 6:38), Hakikisha Mahusiano Yako Na Wazazi Wako Wa Kiroho Yako Sawa (Waefeso 6:1), Linda Uhusiano Wako Na Wazazi Wako Wa Kimwili; Baba Na Mama (Waefeso 6:2-3).
Wekeza Pesa Yako Na Nguvu Yako Kwenye Kazi Ya Mungu (Unamkumbuka Kornelio, Matendo 10? Unamkumbuka Dorkasi, Matendo 9:36-42? Unamkumbuka Mfalme Hezekia, Isaya 38?).
KAZI NI KWAKO; UFALME WA MUNGU UNATEKWA NA WENYE NGUVU!

2.NGUVU ZA KIAKILI/ NGUVU ZA UFAHAMU

Hizi Ni Nguvu Za Kiakili Na Kiufajhamu Atoazo Mungu Kwa Mtu Wake, Ili Aweze KUBUNI, KUWAZA NA KUFIKIRIA Vitu Ambavyo Vinahitajika Kwenye Maeneo Yaliyomzunguka.
Hii Ni Nguvu Ya Kimungu Inayofungua MACHO YAKO YA MOYONI Ili Uweze KUONA FURSA Za KIUCHUMI NA KIMAENDELEO Ambazo Wengine Waliokuzunguka HAWAZIONI!
Mungu Akikupatia Nguvu Ya KIAKILI; Ufahamu Wako Unafunguliwa, Na Unaweza Kuona Zaidi Ya Macho Haya Mawili Yaonavyo.
Unajikuta Umepata UWEZO Wa Kuona Yasiyokuwepo Lakini Yanayoweza Kuwepo. Na Kama Ukichukua Hatua Kuyatendea Kazi Yanageuza Kabisa MAISHA YAKO Kabisa.
Hii Ndiyo NGUVU YA KIAKILI Aliyompa BEZAREL MWANA WA HURI (Kutoka 31: 1-11).
Hii Ndiyo NGUVU YA KIAKILI Aliyompa DANIEL, SHEDRACK, MESHAKI NA ABEDNEGO (Daniel 1:17).
Hii Ndiyo NGUVU YA KIAKILI Aliyompa Nuhu Wakati Wa Kutengeneza Safina (Mwanzo 6:13-16,22).
Hii ndiyo NGUVU YA KIAKILI Aliyompa “MWENYE HEKIMA MASIKINI” Aliyeuokoa Mji Wake Usiangamizwe (Mhubiri 9:13-15).
KUSUDI LA MUNGU KUTUPA ROHO MTAKATIFU WAKRISTO WA SIKU HIZI ZA MWISHO NI ILI AINA HII YA AKILI YA KIMUNGU IWE NASI NA TUWEZE KUFANYA MAMBO MAKUBWA; MAMBO AMBAYO MACHO HAYAJAWAHI KUONA, WALA MASIKIO HAYAJAWAHI KUSIKIA, MAMBO AMBAYO HAYAJAWAHI KUINGIA KWENYE MIOYO YA WANADAMU WENGINE… TUMEPEWA ROHO WA MUNGU, MAKUSUDI “TUYAJUE” YOTE TULIYOKIRIMIWA NA MUNGU (TULIYOKWISHAPEWA NA MUNGU KWA UKARIMU WAKE)… (1Wakorintho 2:9-12)!

3.NGUVU YA MWILINI

Hii Ni Aina Ya Tatu Ya Nguvu Atoayo Mungu. Hii Ni Aina Ya Nguvu Inayohusika Na Kuweka Kwenye Utendaji Kile Ambacho AKILI NA UFAHAMU Vimeamua Kufanya.
Ni Nguvu Ya Kawaida Ya Mwili Ambayo Inakuwa Ndani Ya Mwili Wa Mtu Ili Kuusaidia Mwili Wake UTENDE KAZI ZAKE BILA TATIZO. Yaani Ni Ile Nguvu Ya Kiutendaji Ya Kila Siku Ya Mwili Ambayo Ni Matokeo Ya Kuwa AFYA IMARA NA TIMAMU!
Mungu Kwa Kujua Umuhimu Wa Afya (NGUVU YA MWILI) Aliwahakikishia Waisraeli Walipokuwa Wakienda Kanaani Ya Kuwa “ATAONDOA UGONJWA KATI YAO” (Kutoka 23:25), Kama Haitoshi Alisema “ATAKUWA MPONYAJI WAO” (Kutoka 15:26).
Nasi Kwenye AGANO JIPYA; Ameyatia MAGONJWA NA UDHAIFU WETU JUU YA MWILI WA YESU (Mathayo 8:17), Ili Ugonjwa Na Maradhi Visiwe Vizuizi Vya Afya Zetu Kiasi Cha Kutuzuia “KUFANIKIWA KATIKA MAMBO YETU YOTE NA KUWA NA AFYA KAMA ROHO ZETU ZIFANIKIWAVYO” (3 Yohana 1:2).

Wewe Ndiwe Uliyeshika Fnguo Za Mafanikio Yako; Nguvu Hizo Tatu Ziletazo Utajiri Umezijua, Ni Wajibu Wako KUZIJUA KWA KINA NA KUZITUMIA Kutoka Kwenye Umasikini Wako!

ANGALIZO; Hizi Kanuni Nilizoweka Hapa, Zinaweza Kugeuza Hali Yako Ya Uchumi Kama Utachukua Hatua Kutenga Muda Na Kulisoma Tena Somo Hili Mara Nyingi Uwezavyo; SOMA MISTARI YOTE KWA BIBLIA YAKO, ILI UJIONEE KILA KITU SAWA NA NENO LILIVYOSEMA; Kisha Anza Kutendea Kazi Kwenye Maisha Yako ya Kila Siku!

Pastor D.C.Kabigumila
August 3, 2012.
(Huu ni ufunuo wa Neno la Mungu wa August 03, 2012, miaka karibu 7 iliyopita, ambao ninaona moyoni mwangu, utakufaa sasa tena walau kuamsha kitu ndani yako ili uweze kupiga hatua fulani kwenye eneo la KUTAWALA UCHUMI)

MAMBO MENGINE AMBAYO YANAAMBATANA NA NGUVU ZA KUPATA UTAJIRI:

i) Hakikisha una kazi ya kufanya (una kitu cha kufanya),

Maandiko yanasema, tuhakikishe TUNA KITU CHA KUFANYA KWA MIKONO YETU ILI TUWEZE KUPATA MAHITAJI YETU NA KUPATA CHA KUWAGAWIA WAHITAJI (Waefeso 4:28), pia maandiko yanasisitiza KILA MTU AWE NA KAZI YAKE MWENYEWE, ALE CHAKULA CHAKE MWENYEWE (ALE KWA KUZALISHA NA KUFANYA KAZI NA ASIWE TEGEMEZI) NA ASIYEPENDA KUFANYA KAZI, KULA NA ASILE (2Wathesalonike 3:8-12)!
Katika KILA KAZI KUNA FAIDA (Mithali 14:23).
Wote waliofanikiwa ni WATU WA KAZI! Ni aidha WANATOA HUDUMA FULANI KWA JAMII ambayo jamii inawalipa kwa hiyo au WANAUZA BIDHAA ZINAZOHITAJIWA NA JAMII!
Huwezi kufanikishwa kiuchumi na Mungu BILA KAZI!
Ibrahimu alikuwa na MIGODI YA MADINI YA DHAHABU NA MADINI YA FEDHA, NA ALIKUWA MFUGAJI MKUBWA kupitia hayo MUNGU AKAMTAJIRISHA (Mwanzo 13:2)!
Isaka ALILIMA MWAKA ULE MMOJA, tena kwa kutumia KILIMO CHA UMWAGILIAJI KWA KUFUFUA VISIMA VYA IBRAHIM BABA YAKE VILIVYOFUKIWA NA AKAWA TAJIRI KULIKO TAIFA ZIMA LA GERARI KWA SABABU BWANA ALIBARIKI KAZI YAKE (Mwanzo 26:12-22)!
AYUBU ALIKUWA MTU MKUU KIUCHUMI NA KIROHO KULIKO WATU WOTE WA MASHARIKI (Ayubu 1:1-10)!
Lakini HAIKUTOKEA TU, ALIKUWA NI MTU WA KAZI SANA, HAKUWA MVIVU ANAYEOMBA NA KUSUBIRI VITU VITOKEE KIMIUJIZA BILA KUCHUKUA HATUA KUPIGA KAZI ILI KUZISUKUMA BARAKA TOKA ROHONI KUJA MWILINI!

Alikuwa na NGAMIA AMBAO WALITUMIKA KUFANYA BIASHARA ZA USAFIRISHAJI MIZIGO, KWA SASA TUNAWEZA KUSEMA ALIKUWA NA KAMPUNI YA USAFIRISHAJI!
Alikuwa na JOZI MIA TANO ZA NG’OMBE ambao walitumika KULIMA, hawa tunaweza kusema ALIKUWA NA MATREKTA MIA TANO YA KULIMIA, ALIKUWA LARGE SCALE FARMER, HAKUWA MVIVU NA GOIGOI KAMA WALOKOLE WENGI WA SASA!

Alikuwa na PUNDA WA KUTOSHA KWA AJILI YA KUSAFIRISHA BIDHAA ZAKE KUZIPELEKA MASOKONI NA KUKODISHA WENGINE WENYE HAJA YA USAFIRI!
Naamini unaelewa kwanini MABABA HAWA WA IMANI WALIKUWA NA UCHUMI MZURI, NA SISI WA SASA TUNATOA TU MACHO NA KUNG’AA SHARUBU BILA MATOKEO!
TUMEIPUUZA KANUNI YA KAZI tukidhani MAOMBI NA SADAKA BILA KUPIGA KAZI KWA VIWANGO NA BIDII vitaleta utajiri na ustawi kiuchumi, TUREKEBISHE HAYA MAKOSA!

ii) Hakikisha una bidii kwenye kazi zako
-Epuka kulala kuzidi masaa 6 kwa siku
-Epuka uvivu na uzembe
-Epuka kufanya vitu kwa kujivuta au kusukumwa sukumwa
-Epuka kuahirisha ahirisha vitu ukisema na kesho ipo nitafanya, LINALOWEZEKANA LEO LISINGOJE KESHO, FANYA VITU IN ADVANCE!
-Panua ufahamu wako na uelewa wako kuhusu kila bidhaa au huduma unayotoa kwa jamii ili iwe pesa, hakikisha unakuwa mbunifu na mtu wa ubora!

iii) Kaa vizuri na watu

-Watu ndio wanaamua maisha yetu yatafika wapi (Isaya 43:4)
-Kadri unavyogusa maisha ya watu, wao pia wataguswa kukupa kipimo cha kujaa, kushindiliwa na kusukwa sukwa (Luka 6:38),
-Watu wana utajiri wako na pesa yako (Isaya 60:11),
-Ukiwa na watu wa kutosha walio sahihi, utafanikiwa kwa urahisi kuliko ukiwa na uhaba wa watu (Mithali 14:28).

MAOMBI

1. MUOMBE MUNGU AKUPE NGUVU ZA KIROHO ZA KUPATA UTAJIRI

i) Ideas (Mawazo) ya kukutoa ulipo na ya nini ufanye
ii) Nguvu ya kuanza vitu na kumaliza
iii) Nguvu ya uthubutu na kuchukua hatua
iv) Nguvu ya kutiisha kila upinzani na nguvu zizuiazo
v) Nguvu ya Kibali
vi) Nguvu ya kukua, kuenea na kutawala

2. MUOMBE MUNGU AKUPE AKILI NA UFAHAMU BORA
-Kutoka 31:1-10, Danieli 5:10-14, 2Timotheo 2:7, Danieli 1:17, 1Wafalme 4:29

3. MUOMBE MUNGU NGUVU YA KUTUNZA MWILI WAKO

i) Akili na hekima ya kuepuka na kujidhibiti ulaji wa vyakula ambavyo haviongezi kitu mwilini kama soda, mayai ya kisasa, kuku wa kisasa, utumiaji wa sukari kupita kiasi, uvivu wa kunywa maji, uvivu wa kufanya mazoezi, utumiaji vipodozi na kemikali zisizofaa za ngozi na mengine mengi ambayo siku hizi yameongezeka kwa sababu ya watu wengi kuwa CARELESS NA MAISHA YAO KWA KISINGIZIO CHA KUWA BUSY!

ii) Jaza Neno la Mungu kuhusu afya ya kiungu na kwanini usiwe mgonjwa (TAFUTA YOUTUBE VIDEO ZANGU ZA KWANINI MTU AKIOKOKA HAPASWI KUWA MGONJWA- Zinapatikana channel ya Pastor Dickson Cornel Kabigumila), tafuta vitabu vya Dr. David Oyedepo, Kenneth E Haggin na Pastor Chris Oyakhlome wote hawa wamenijenga kwenye ENEO LA KUTEMBEA NA AFYA YA KIUNGU (DIVINE HEALTH)!

iii) Utunze mwili wako maana huo ndio unaamua utakaa kiasi gani duniani ndani yake! Mwili wako ni hekalu la Roho Mtakatifu, usiuharibu na kuutumia kufanya vitu kama uzinzi, uasherati, unywaji wa pombe, uvutaji sigara, utumiaji madawa ya kulevya, kulala kupita kiasi (zaidi ya masaa 6 kwa siku), au kulala pungufu ya masaa walau 5 kwa siku, UHESHIMU MWILI WAKO, NAO UTAITUNZA ROHO YAKO.

iv) Kuwa mtu wa mifungo ya kutosha, ITATUNZA MNO AFYA YAKO, maana kuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya KUWA NA AFYA NZURI NA UFUNGAJI (Soma Isaya 58:1-12 utaona).
Mtu anayefunga, AFYA YAKE ITAKUJA MARA!
Mtu anayefunga, ATAJAA NURU KWENYE AKILI, ROHO NA MWILI WAKE!
Mtu anayefunga, ATAKUWA KAMA BUSTANI ILIYOTIWA MAJI!
BE A FASTING MACHINE, huku ukizingatia mno yale matatu niliyosema hapo juu, nawe utakuwa mtu mwenye AFYA SAFI itakayopelekea utafutaji na harakati za maisha kwenda vizuri!

 

Usiache kutembelea website yangu ya www.yesunibwana.co.tz na kuweka email yako (kujiunga), ili tuwe tunakutumia masomo walau mara mbili au tatu kila wiki!

NDOA

“Haiunganishi familia mbili bali inazalisha familia mpya ya tatu… Inayojiendesha, kujitawala, kujiamulia na kujichagulia mambo yake… Familia hii mpya ya tatu inakuwa na kusudi na

Read More »

HEKIMA ZA NDOA 4

“Ndoa ni taasisi ambayo unaungana na mtu mwingine ambaye ANAWEZA KUKUTIA MOTO kwenye KULIFUATA NA KULITIMIZA KUSUDI LA MUNGU… Wawili sahihi kila mmoja anakuwa CHUMA

Read More »