NGUVU YA MCHUNGAJI MMOJA TU ALIYEPATA NEEMA YA KUANDALIWA NA MUNGU

Huwa ninajiuliza NGUVU YA MCHUNGAJI MMOJA TU ALIYEPATA NEEMA YA KUANDALIWA NA MUNGU NA MIKONO YA WATU SAHIHI…

Huwa nachukulia mfano mmoja tu dhaifu wa MIMI TU MMOJA AMBAYE NINASUA SUA, MNYONGE NA ASIYE NA UWEZO KABISA, na vile NAMNA MUNGU AMEYATUMIA MAISHA YANGU KUWA NA KULETA NURU…

Huwa nawaza sana kwamba mfano Mungu akanisaidia KUTENGENEZA WACHUNGAJI 100 TU AINA YA DICKSON CORNEL KABIGUMILA kabla ya kuondoka huku duniani…

Yaani wawepo WACHUNGAJI 100 walio na kiuwezo kidogo cha kiroho, kiakili, kimaamuzi, kimaono, na kiutendaji katika Kristo kama DICKSON CORNEL KABIGUMILA alivyo tu walau…

Maana yake tungekuwa walau KILA MKOA MMOJA WA TANZANIA una AKINA KABIGUMILA 3, wanaojaribu jaribu, na kufanya walau tu kwa kiwango kiduchu mno cha ABC GLOBAL,

Kwa unyenyekevu wote kwa Mungu na kwako msomaji, NAAMINI HATA HALI YA NCHI INGEBADILIKA SANA, kwa sababu walau WANANCHI MILIONI KADHAA WANGECHUNGWA NA KULELEWA KWA UTARATIBU UNAOELEWEKA NA KUJA KUWA CHACHU YA TANZANIA BORA AMBAYO HUENDA ITABAKI PRAYER POINT TU TUSIPOANZA KUIZAA NDANI YA WASHIRIKA WETU…

Ninafahamu kuwa, KIWANGO CHA JUU CHA UFALME NI WATU KUKUA NA KUFIKIA KIMO CHA KRISTO ALIYE BWANA NA KICHWA CHA KANISA, LAKINI MIMI NIMEWAAMBIA WATU WA ABC GLOBAL, WAKATI WANAKAZANA KUWA KAMA KRISTO, WAANZE NA KIWANGO CHA CHINI CHA KINYONGE SANA CHA KUWA KAMA DICKSON CORNEL KABIGUMILA…

Hii ni kwa sababu, WALAU KATIKA UNYONGE, UDHAIFU, UKAWAIDA SANA NILIONAO, KUNA ALAMA ISIYOWEZA KUFUTIKA NIMESHAIWEKA KWA MAARIFA, UFAHAMU NA HEKIMA YA NENO LA MUNGU KIDOGO NILIYOWEZA KUIKUSANYA NA KUIISHI, NA BAHATI NJEMA KILA KITU NINACHOKIJUA HUWA NASHARE HAPA HAPA MITANDAONI NA KWENYE MAFUNDISHO YANGU KWA UWAZI…

LENGO LANGU NI NINI?

  1. Kama ni mwana ABC GLOBAL, kazana sana kufikia tu hapa padogo ambapo BABA YAKO NILIYE MDOGO KULIKO WOTE nimefika, ISHI TU YALE AMBAYO NIMEYAISHI, NIMEYAFANYA, NA KUKUFUNDISHA KWA MIAKA ULIYONIFAHAMU, YAMESHATHIBITISHWA NA NENO NA MUDA KWAMBA YANAFANYA KAZI
  2. Ni muhimu sana KUWA KAMA KRISTO, lakini kabla ya KUFIKIA LENGO HILO KUU MNO, jitahidi sana UWE KAMA BABA YAKO KATIKA KRISTO ikiwa ana cha kuonyesha kama zao la yeye KUMFUATA KRISTO NA KANUNI ZA UFALME
  3. Nimejiridhisha bila shaka ya kuwa KUTENGENEZA WATU WENYE UWEZO NA UBORA WALAU KAMA WAKO NA KUWAONESHA NAMNA YA KUKUPITA NA KUWA ZAIDI YAKO, NDIYO NJIA YA UHAKIKA YA KUINUNUA KESHO KWENYE HUDUMA AU TAASISI YOYOTE

Nisikuchoshe sana na maneno yangu,
Wale wasiopenda kujifunza wanadai ninajisifu na mimi sitaki kuwakwaza maana kivuli cha maisha yao kinawahukumu na lawama wanataka kunipa mimi,
Askofu Dickson Cornel Kabigumila
ABC GLOBAL
05.11.2024

Mafundisho
yesunibwana

SEX BEFORE MARRIAGE

#TENDO LA NDOA KABLA YA #NDOA Luka 16:10 [10]Aliye mwaminifu katika lililo dogo sana, huwa mwaminifu katika lililo kubwa pia; na aliye dhalimu katika lililo

Read More »

NDOA

“Haiunganishi familia mbili bali inazalisha familia mpya ya tatu… Inayojiendesha, kujitawala, kujiamulia na kujichagulia mambo yake… Familia hii mpya ya tatu inakuwa na kusudi na

Read More »
Mafundisho
yesunibwana

SIFA ZA MME BORA

  1. Yeye mwenyewe AMEMPOKEA YESU, NA KUJITIA CHINI YA MAMLAKA YAKE KAMA BWANA NA MWOKOZI WAKE KIBINAFSI (Yohana 1:12-13, Yohana 3:16-18). -Atambue thamani ya

Read More »