ADUI ANAFANYAJE KAZI?

ADUI ANAFANYAJE KAZI?

2 Samweli 17

1 Zaidi ya hayo Ahithofeli akamwambia Absalomu, Niache nichague watu kumi na mbili elfu, nami nitaondoka na kumfuatia Daudi usiku huu;

2 nami nitamshambulia wakati atakaokuwa amechoka, na mikono yake imekuwa dhaifu, nami nitamtia hofu; na watu wote walio pamoja naye watakimbia; nami nitampiga mfalme peke yake;

1. Anasubiria kwanza apate nafasi ambayo mhusika hajajipanga au kujiandaa kwa shambulio la ghafla

“Nitaondoka na kumfuatia Daudi usiku huu”

Wanajua akitulia usiku mzima akapata usingizi mzuri, akawaza na kuwazua, kesho atakuwa amerudi kwenye ubora wake, na hawataweza kumshinda wala kumuua!

Wala usimpe Ibilisi nafasi kama hii ya kukushambulia ghafla- Waefeso 4:27

Kila muda unaoona kuna amani, mafanikio, huduma inachanua, kila kitu kinakuendea vizuri kwenye ndoa, biashara au kazini, huo ni wakati wa hatari zaidi rohoni- 1Thesalonike 5:3

2. Wanasubiri uchoke kwanza

“Nami nitamshambulia wakati atakaokuwa amechoka…”

• Uchoshwe na mafanikio madogo uliyoyapata kwa taabu mno

•Uchoshwe na kupambana lakini matokeo hakuna au hayaridhishi, na ubaki njia panda

Vyote viwili hapa juu hutumiwa na Shetani kama dalili au ishara ya kuwa mhusika anapigika sasa,

Usikubali kuchoka, endelea kusukuma, endelea kupambana kama hakijatokea kitu, na kuzimu haitakushinda!

3. Mikono yako inapokuwa dhaifu

“…Na mikono yake imekuwa dhaifu…”

Mikono inawakilisha nguvu

Mikono inawakilisha kile unachofanya na kikakupa kuwa na nguvu rohoni,

Yawezekana ni maisha matakatifu,

Yawezekana ni maombi mengi,

Yawezekana ni mifungo mirefu,

Yawezekana ni utoaji wa bila kujihurumia,

Yawezekana ni mikesha binafsi kanisani kila wiki,

Yawezekana ni kujitenga na vitu vinavyokula moto wa Mungu kama michezo, comedy, movies nk

Wakikutoa kwenye “mikono kuwa na nguvu” ukawa dhaifu kwa kuyaacha haya, UJUE UNAKARIBIA MNO KUSHAMBULIWA NA KUPIGWA NA ADUI!

4. Hofu ni silaha ya Shetani ya muhimu mno dhidi yako

“…Nami nitamtia hofu…”

Mtu akibaki na ujasiri wake, hakuna Shetani au giza litamshinda!

Atakuangusha kwenye dhambi na uovu ili upoteze ujasiri ili akushambulie kwa wepesi,

Hofu ni mlango mkuu wa kipepo wa kumshinda mtu!

Lakini atukuzwe Mungu kwa sababu;

2 Timotheo 1

7 Maana Mungu hakutupa roho ya woga, bali ya nguvu na ya upendo na ya moyo wa kiasi.

5. Atakutenga kwanza na watu ambao wanakupenda kweli, wanaokuombea kweli, ataondoa watu wa maana wote ili ubaki mwenyewe akukung’ute vizuri!

“Nami nitampiga mfalme atakapobaki peke yake”

Shetani atakuondolea ulinzi wa watu waaminifu na waadilifu kwako, ndipo atakupiga ukiwa huna tena wa kukuombea au kukusaidia!

Kila ukiona watu wakweli, wanaokupenda kwa dhati wanaondoka maishani mwako, ujue Shetani anajipanga kukumaliza!

Askofu Dickson Cornel Kabigumila

ABC GLOBAL

Mafundisho
yesunibwana

KWA WAOLEWAJI TU

“Kati Ya Mambo Unayopaswa Kuyachunguza Kuhusu Mtu Anayetarajia Kukuoa NI UAMINIFU NA UADILIFU Kwenye MALI NA PESA YA UMMA, KAMPUNI Au WATU WENGINE… Ukiona Huyu

Read More »

HEKIMA ZA NDOA 4

“Ndoa ni taasisi ambayo unaungana na mtu mwingine ambaye ANAWEZA KUKUTIA MOTO kwenye KULIFUATA NA KULITIMIZA KUSUDI LA MUNGU… Wawili sahihi kila mmoja anakuwa CHUMA

Read More »

HEKIMA ZA NDOA 3

  “Kusudi la ndoa ni kujenga TIMU YA WANAOSADIANA NA KUINUANA. Wawili ni bora kuliko mmoja, MAANA MMOJA AKIANGUKA, MWENZIE ATAMUINUA. Ndoa sahihi ni muunganiko

Read More »