MFUNGO WA SIKU 10,MASAA 12 -AUGUST [SIKU YA 2]

NGUVU YA KUANZA MAMBO MAPYA (THE POWER TO START NEW CHAPTERS).

Maandiko:

“Bali njia ya wenye haki ni kama nuru ing’aayo ikizidi kung’aa hata mchana mkamilifu. Njia ya waovu ni kama giza; Hawajui ni kitu gani kiwakwazacho”
(Mhubiri 4:18-19).

“Nawe utakusudia Neno (Utatamka vitu), nalo litathibitika kwako; Na mwanga utaziangazia njia zako. Hapo watakapokuangusha, utasema, KUNA KUINUKA TENA; Naye mnyenyekevu Mungu atamuokoa”
(Ayubu 22:28-29).

“Kwa maana mwenye haki huanguka mara saba AKAONDOKA TENA; Bali wasio haki hukwazwa na mabaya”
(Mithali 24:16).

“Lakini mimi, nitamtazamia Bwana; nitamngojea Mungu wa wokovu wangu; Mungu wangu atanisikia. Usifurahi juu yangu, Ee adui yangu; NIANGUKAPO NITASIMAMA TENA; Nikaapo gizani, Bwana atakuwa nuru yangu…ATANILETA NJE KWENYE NURU, NAMI NITAIONA HAKI YAKE. Ndipo adui yangu ataliona jambo hilo, na aibu itamfunika…”
(Mika 7:7-10).

“Msiyakumbuke mambo ya kwanza, wala msiyatafakari mambo ya zamani. Tazama, NITATENDA NENO JIPYA; SASA LITACHIPUKA…”
(Isaya 43:18-19).

“Na mataifa wataiona haki yako, na wafalme wote watauona utukufu wako; NAWE UTAITWA JINA JIPYA, LITAKALOTAJWA KWA KINYWA CHA BWANA”
(Isaya 62:2).

“Angalia siku zinakuja, asema Bwana, NITAKAPOFANYA AGANO JIPYA na nyumba ya Israeli, na nyumba ya Yuda”
(Yeremia 31:31).

“…tena hayo ya zamani mtayatoa, ILI MUYAWEKE YALIYO MAPYA”
(Walawi 26:10).

“Tazama, mambo ya kwanza yamekuwa, NAMI NAYAHUBIRI MAMBO MAPYA; KABLA HAYAJATOKEA nawapasha habari zake”
(Isaya 42:9).

“Umesikia haya; tazama haya yote; nanyi, je hantayahubiri? NIMEKUONYESHA MAMBO MAPYA TANGU WAKATI HUU, NAAM MAMBO YALIYOFICHWA, USIYOYAJUA”
(Isaya 48:6).

“NAYE ATAFUTA MACHOZI KATIKA MACHO YAO, wala mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo tena; KWAKUWA MAMBO YA KWANZA YAMEKWISHA KUPITA. Na yeye aketiye juu ya kiti cha enzi akasema, TAZAMA NAYAFANYA MAMBO YOTE KUWA MAPYA. Akaniambia, Andika ya kwamba maneno hayo ni amini na kweli. AKANIAMBIA, IMEKWISHAKUWA…”
(Ufunuo 21:4-6).

Mambo ya kujifunza;

1. Maisha ni kitabu chenye kurasa nyingi, na Mungu ametupa nafasi ya kugeuza kurasa mbaya na ngumu kwa MANENO YETU ili kupata KURASA MPYA tutakazo.
(Ayubu 22:28-29, Mika 6:1).

2. Hakuna jambo baya lisiloweza kubadilika endapo mhusika atakubali KUYASAHAU YALIYOPITA na kumruhusu Mungu amsaidie kutengeneza ukurasa mpya ulio bora.
(Isaya 43:18-19).

3. Hakuna jambo jipya linalotokea kwa bahati mbaya, ni lazima mhusika AAMINI KATIKA JAMBO JIPYA, NA AANZE KUPAMBANA KUELEKEA MAHALI PA MUUJIZA WAKE!

Uamuzi wa kuendelea kukaa kwenye mambo mabaya yaliyopita au kuinuka na kusimama viko mikononi mwa mtu, akikubali kusimama, mbingu zinamsaidia!
(Mika 7:7-10, Mithali 24:16).

4. Mungu ni bingwa wa kuumba mambo mapya kokote, saa yoyote akiruhusiwa tu na IMANI YA MTU.

*Tumbo LILILOKUFA LA SARA LILIZAA!

*Taya la punda mikononi mwa Samson liliua askari elfu moja.

*Jiwe moja dogo liliua jitu Goliati aliyeogopwa na jeshi kwa siku 40.

JAMBO JIPYA HALIKO MBALI NA MTU, AKIWEZA KULIONA NDANI YAKE ATALIPATA NJE!

5. Kila hali ngumu anayopitia mtu dawa yake ni JAMBO JIPYA, ambalo hakika Bwana Yesu anaweza kulifanya!
(Ufunuo 21:3-6).

MAMBO YANAYOSABABISHA JAMBO JIPYA LICHIPUKE;

1. Kuyaacha na kutoyapa nafasi yaliyopita.
(Isaya 43:18-19).

2. Kumuamini Mungu kwa ajili ya kesho bora kuliko jana yako.
(Mithali 4:18, Ayubu 8:7).

3. Kutamka maneno ya kuliumba jambo jipya katikati ya jambo baya unalopitia.
(Mika 6:1, Mika 7:7-8, Ayubu 23:10).

4. Kujua kwamba nyakati mbaya na ngumu NI MAPITO KWENYE MAISHA NA HAZIDUMU bali Uaminifu wa Mungu wadumu milele!
(Zaburi 23:4-6, 2Wakorintho 4:16-18).

MAOMBI

Asubuhi

1. Omba nguvu ya kuinuka tena kutoka katika kila hali, changamoto, jaribu au ugumu uliokuwa unaupitia.
( Zaburi 118:5, Yona 2:2).

2. Omba uwezo wa kuamini katika nguvu za Mungu za kufanya mambo mapya.
(Mwanzo 18:14, Luka 1:37).

Mchana

1. Omba Mungu akupe uwezo wa kuyasahau mabaya, maovu na mazito uliyopitia, na kuinua imani ya kupokea mapya aliyokuandalia.
(Ufunuo 21:4-6, Isaya 43:18-19).

2. Muombe Mungu adhihirishe nguvu ya agano jipya maishani mwako;
Mahali pa huzuni na masikitiko yatoweke.
(Isaya 53:4).
Magonjwa yaondoke.
(Mathayo 8:17,1Petro 2:24).
Umasikini unapisha utajiri na mafanikio.
(2Wakorintho 8:9, 3Yohana 1:2).
Aibu na kushushwa vinapisha utukufu na heshima.
(Warumi 8:29-30).

Jioni

1. Mshukuru Mungu kwa ajili yangu mimi Mwalimu Dickson Cornel Kabigumila na kile anachofanya kupitia maisha yangu.
(Zaburi 89:20-37).

2. Mshukuru Mungu kwa kujibu kila uliloomba kwa siku hizi mbili
(Wafilipi 4:6-7).

HONGERA KWA KUSHIRIKI MFUNGO, HUU NA KUHITIMISHA SIKU HII YA PILI KWA USHINDI MKUU, HAKIKA USHUHUDA WAKO UTAKUWA DHAHIRI.
(Zaburi 126:1-2).

U mbarikiwa sana, mbeba majibu ya dunia yako!

TUKUTANE KESHO SIKU YA TATU.

Dickson Cornel Kabigumila,
Mchungaji mwanzilishi,
Assembly Of Believers Church (ABC),

KWA MAFUNDISHO ZAIDI TEMBELEA TOVUTI YANGU HII:
www.yesunibwana.co.tz

YOUTUBE: Tafuta Channel hizi

CHURCH STATION

PASTOR DICKSON CORNEL KABIGUMILA

INSTAGRAM:
@mwalimukabigumila

Mafundisho
yesunibwana

WAZEE WA MKEKA/KUBETI MPOO!!

  USHUHUDA: AFUNGULIWA TOKA TABIA SUGU YA KUCHEZA KAMARI, MAARUFU KAMA KU-BET AU KUTANDIKA MIKEKA! Ngoja nikupe mchongo wa kukutoa jumla kwenye huu MSALA. Huu

Read More »

USIOE KWA SABABU :2

  “Wenzako wote uliokua nao au kusoma nao wanaoa. Ndoa si ALISEREMA ARIJA AU MWENGE TUNAUKIMBIZA. Ndoa ni taasisi ambayo Mungu amemuwekea kila mmoja wetu

Read More »

HEKIMA ZA NDOA 5

“Ni mwanandoa mpumbavu pekee anayesubiri aombwe msamaha ili asamehe; Maana waweza kukuta kile unachoona kama kosa, mwenzako anaweza asikione hivyo, kwa kutosamehe ufa huo unaweza

Read More »
Mafundisho
yesunibwana

SEX BEFORE MARRIAGE

#TENDO LA NDOA KABLA YA #NDOA Luka 16:10 [10]Aliye mwaminifu katika lililo dogo sana, huwa mwaminifu katika lililo kubwa pia; na aliye dhalimu katika lililo

Read More »