MFUNGO MAALUM WA SIKU KUMI [SIKU YA 7]- JULAI 2019

MAFANIKIO YA KIUCHUMI KWA MIEZI SITA IJAYO

Utangulizi

Ni mapenzi ya Mungu TUFANIKIWE KIUCHUMI (3Yohana 1:2)!

Mungu anataka kuona KILA TUFANYALO LIKIFANIKIWA (Zaburi 1:3)!

Mungu anataka kuona KATIKA KILA SHUGHULI YETU YA UZALISHAJI (KAZI) TUNAPATA FAIDA (Mithali 14:23).

Mungu anataka kutupatia NGUVU ZAKE ZINAZOFANYA WATU WAKE WATAJIRIKE NA KUSTAWI KIUCHUMI (Kumbukumbu 8:18)!

Mapenzi ya Mungu kwetu ni SISI KUJENGA NYUMBA NZURI (NA SI BORA NYUMBA) NA KUKAA NDANI YAKE… FEDHA YETU IONGEZEKE NA SI KUFILISIKA… DHAHABU YETU (MALI) IONGEZEKE… WANYAMA (MIFUGO) WAONGEZEKE… NA KILA TULICHONACHO KIONGEZEKE ILI MRADI TU TUMEDHAMIRIA MIOYONI MWETU YA KUWA MAFANIKIO NA USTAWI KIUCHUMI HAVITAIVURUGA IMANI YETU KWAKE NA KUTUNYIMA NAFASI YA KUMPENDA NA KUMTUMIKIA (Kumbukumbu 8:11-17)!

Mungu wetu anataka SISI WANA WA IBRAHIM tuwe MATAJIRI SANA KAMA IBRAHIM BABA YETU ALIVYOKUWA TAJIRI KATIKA DHAHABU (MIGODI YA DHAHABU), MIFUGO NA FEDHA (MIGODI YA SILVER): Mwanzo 13:2!
Maana wale tulio wa imani, tu wana wa Ibrahim na warithi wa KILA AHADI NA BARAKA YAKE (Wagalatia 3:7, Wagalatia 3:9).
Kupitia kifo cha Bwana Yesu msalabani, BARAKA YA IBRAHIM NI HAKI YA KILA ALIYEOKOKA, AKITAMBUA HILO NA KUAMINI/ KWA NJIA YA IMANI (Wagalatia 3:13-14)!
Ukishakuwa WA KRISTO (MALI YA KRISTO) KUPITIA WOKOVU, WEWE NI MWANA WA IBRAHIM NA UNAPASWA KUFANIKIWA NA KUSTAWI KIUCHUMI KAMA IBRAHIM (Wagalatia 3:26, Wagalatia 3:29).

Lakini ili UPATE MATOKEO YA IBRAHIM, LAZIMA UFANYE KAZI ZA IBRAHIM, YAANI UFANYE VITU (MATENDO) YA IMANI YALIYOMPELEKEA AKASTAWI KIUCHUMI!
Yesu alisema, IKIWA SISI NI WANA WA IBRAHIM, TUFANYE KAZI ZAKE IBRAHIM (Yohana 8:39)!

Kwenye Kitabu cha Isaya 51:2, MUNGU ANASEMA NA WAZAO WA IBRAHIM WENYE LENGO LA KUSTAWI KIUCHUMI akisema:

“MWANGALIENI IBRAHIM, BABA YENU, NA SARA, ALIYEWAZAA; KWA MAANA ALIPOKUWA MMOJA TU (UCHACHE, UPUNGUFU, BILA JINA) NALIMWITA, NIKAMBARIKI NA KUMFANYA KUWA WENGI”

Anaposema, *”Mwangalieni Ibrahim”* ana maanisha:
i) Fanya study ya maisha ya Ibrahim
ii) Tafuta siri za maisha ya IBRAHIM zilizomfanya awe tajiri
iii) Angalia vitu vilivyopelekea Ibrahim akafanikiwa kiuchumi ingawa Mungu alimuita akiwa mmoja (uchache) na akambariki na kumfanya wengi (utele)
iv) Kagua mambo aliyofanya Ibrahim yaliyofungua mlango wa MBINGU kugeuza maisha yake

NITAKUSAIDIA SIRI HIZO, LAKINI UAMUZI WA KUZIFANYA ILI ZIGEUZE MAISHA YAKO UNABAKI MIKONONI MWAKO!
MIMI NILIZIJUA SIRI HIZI MAPEMA, NA NILISHAANZA KUZIISHI KITAMBO!
JAPOKUWA SI MILIONEA AU BILIONEA SASA, LAKINI NIKO MBALI KIUCHUMI NA NINA USTAWI KWENYE MAENEO YOTE (KIROHO, AFYA, FAMILIA, HUDUMA NK)!

SIRI ZA IBRAHIM ZILIZOMFANYA ASITAWI:

i) Ibrahim alimwamini Mungu bila mashaka na bila maswali/ alikuwa mtu wa imani
*”… NAYE IBRAHIM ALIMWAMINI MUNGU…”
(Wagalatia 3:6-9, Warumi 4:3).
ALIAMINI NINI KWA HUYU MUNGU?

•Aliamini kila kitu alichoambiwa na Mungu hata kama kwa nje kilikuwa HAKI-MAKE SENSE!
Mfano Mungu anamuambia tazama angani, ona hizo nyota zote angani, NA KAMA ZILIVYO NDIVYO UZAO WAKO UTAKAVYOKUWA! Naye anajibu SAWA MUNGU WANGU, ni naamini na itakuwa hivyo!
Hapo tayari NI MZEE, HANA UWEZO NA NGUVU YA KUZALISHA, NA MKEWE SARA TUMBO LAKE LIMEKUFA, HALINA TENA OVARI ZA KUZAA WATOTO, lakini ANASEMA ILIMRADI MUNGU KASEMA, LAZIMA TUTAPATA WATOTO KAMA NYOTA ZA MBINGUNI (Warumi 4:17-21)!

Mimi na wewe HATUNA IMANI YA NAMNA HII! Ukisoma Ujumbe kama Huu wa leo, UNASEMA NITAKUWA TAJIRI KWA UTUKUFU WA JINA LA YESU, KAMA IBRAHIM, ukikaa wiki moja, HUNA kodi, HUNA CHAKULA, HUNA AJIRA, HUNA BIASHARA, mara unasikia serikali au taasisi zinasema, UCHUMI WA NCHI UMESHUKA KWA ASILIMIA KADHAA, au MZUNGUKO WA PESA NI MBAYA, imani yoooote ya kutajirika INAPOTEZWA NA HUU UPUUZI WA TAARIFA MBAYA ZILIZOTUZUNGUKA!

Ukitaka kuwa tajiri kama IBRAHIM, lazima ujenge msuli wa KUMUAMINI MUNGU ATAJIRISHAYE (Mithali 8:17-21), kuliko TUMBO LILIKOKUFA LA SARA WALA UZEE WA IBRAHIM!
Yaani UBAKI NA NENO TU, NA UISHI KWA NENO TU, UAMKE KWENDA KAZINI KWA NENO TU! UFANYE BIASHARA KWA NENO LA UTAJIRISHO TU!
UFANYE KILA SHUGHULI ZAKO ZA UZALISHAJI UKIWA UMEZIBA MASIKIO DHIDI YA HASARA, KUSUASUA KWA UCHUMI, HALI NGUMU ILIYOKO KWENYE NCHI NA MENGINE AMBAYO WAPAGANI NA WAKRISTO JINA HUYAOGOPA!

HII NDIYO SIRI NAMBA MOJA YA UTAJIRI MKUBWA WA IBRAHIM.
*”ALIMUAMINI MUNGU NA NENO LAKE NA KULIFANYA KUWA DIRA PEKEE YA MAISHA YAKE NA SI KINGINE CHOCHOTE HATA KAMA KINA UHALISIA AU UKWELI WA WAZI KIASI GANI!”*
HII NDIYO SIRI YA USTAWI NA MAFANIKIO YANGU, NA WATUMISHI WENGI WALIOFAULU KWENYE ENEO LA UCHUMI KAMA DR. DAVID OYEDEPO, KENNETH COPELAND, EMMANUEL MAKANDIWA NA KENNETH HAGGIN!

ii) IBRAHIM ALIKUWA MTOA ZAKA (Mwanzo 14:17-20).
-Ni mtu wa kwanza kutoa ZAKA
-Alitoa ZAKA ya VITU VYAKE VYOTE (Yaani, alitoa ZAKA ya kila mradi na biashara bila kujihurumia)

SIKU hizi kuna kelele nyingi hasa mitandaoni kuhusu ZAKA, wengine wakisema SI HALALI KUTOA ZAKA KATIKA AGANO JIPYA!

Mimi nakuambia, KAMA UNATAKA MATOKEO YA IBRAHIM, FANYA ALIYOFANYA IBRAHIM YAKAMFANIKISHA, Achana na kelele za walioshindwa!
TOA ZAKA YAKO BILA MASWALI NA KWA IMANI

Na ZAKA yako ITOE KWA MLEZI WAKO WA KIROHO/ BABA WA KIROHO, usiitoe tu mahali eti kwa vile unahudhuria Jumapili mpaka Jumapili, ITOE KWA MTU AMBAYE NDIYE ANAYELISHA MAISHA YAKO YA KIROHO NA KUKUFANYA UKUE NA KUSTAWI KUPITIA MAFUNDISHO YAKE, USHAURI WAKE NA HEKIMA YA MUNGU ALIYOBEBA!
Ibrahim alitoa ZAKA kwa MELKIZEDEKI kwa kuwa ndiye aliyekuwa AKIMPA MKATE (NENO) NA DIVAI (UPAKO ALIOBEBA MELKIZEDEKI NDIO ULIKUWA UKIYARAHISISHA MAISHA YA IBRAHIM), NA NDIYE ALIYEKUWA AKIMBARIKI NA KUFUATILIA MAISHA YAKE!
Kama unaye mtu wa hivi, anayewajibika kwako hivi, HUYO NDIYE MADHABAHU YAKO YA KUWEKA ZAKA YAKO, HUYO NDIYE MELKIZEDEKI WAKO!
Kama HUNA mtu wa hivi, Muombe Mungu akupatie, huyo mtu analo neno (MKATE) na UPAKO (divai) wa kukuvusha!

iii) IBRAHIM ALIKUWA MTOA MALIMBUKO
Malimbuko ni kile kipato chako cha kwanza!
Kama ni biashara umeifungua, ni faida yote ya kwanza!
Kama ni ajira ni mshahara wote wa kwanza!
Kama ni kilimo, chukua yote uliyopata toa gharama za uzalishaji, faida yote ya msimu wa kwanza ni malimbuko!
Kama ni mifugo, kila mnyama wa kwanza, kwenye kila mradi mpya wa kufuga huyo ni malimbuko!
IBRAHIM ALITOA MALIMBUKO KWA KIWANGO CHA JUU, KIASI CHA KUMTOA MZALIWA WAKE WA KWANZA ISAKA (Mwanzo 22:1-18)!
Maandiko yanasema, *”MHESHIMU BWANA KWA MALI ZAKO NA KWA MALIMBUKO YA MAZAO YAKO YOTE (VYANZO VYAKO VYOTE VYA UCHUMI VITOLEE MALIMBUKO)… halafu, NDIPO GHALA ZAKO ZITAKAPOFURIKA KWA WINGI (MAZIDISHO NA MAONGEZEKO) NA MASHINIKIZO YAKO YATAFURIKA KWA DIVAI MPYA (NEW IDEAS, OVERFLOW OF INSIGHTS)…”*
(Mithali 3:9-10).
Malimbuko si sadaka ya kulazimishwa, ni sadaka ya wale waliopata Ufunuo tu, WALIOONA UMUHIMU NA BARAKA NYINGI ZILIZOJIFICHA NYUMA YA SADAKA HII!
Baada tu ya IBRAHIM kutii na kutoa MALIMBUKO yaitwayo Isaka, Mungu alishindwa kujizuia akasema, *”SASA NAJUA IBRAHIM YU AMCHA BWANA! KATIKA KUBARIKI NITAKUBARIKI NA KATIKA KUZIDISHA NITAKUZIDISHA…”* (Mwanzo 22:15-18).
Hii ilikuwa TURN AROUND YA UCHUMI WA IBRAHIM!
Kama umeona hii kitu ni muhimu, CHANGAMKIA FURSA, TOA HAYO MALIMBUKO!
FANYA ALIYOKUWA AKIFANYA IBRAHIM, NAWE UTAMU-EXPERIENCE MUNGU ALIYEGEUZA UCHUMI WA BABA YAKO IBRAHIM!

iv) IBRAHIM ALIKUWA AMEFIKA KIWANGO AMBACHO, HAKUWA NA KITU AMBACHO ANAWEZA KUMZUILIA MUNGU AKIMSEMESHA AU KUMGUSA AKITOE (Mwanzo 22:15:17).
-Mungu alitaka GOVI YAKE NA WANAE, akatoa na suala la kutahiriwa likaanzia hapo!
-Mungu alimtaka Isaka hakuuliza maswali
-Mungu alimwambia AMFUKUZE ISHMAEL MWANAE NA MAMA YAKE HAJIRI, hakuwa na maswali, HE SACRIFICED!

Sasa mimi na wewe tunaojiita wenye neema, wa agano jipya, MUNGU AKIKUAMBIA TOA MSHAHARA WAKO WOTE WA MWEZI HUU, utauotoa?

Mungu akikuambia, TOA GARI YAKO KAMPATIE mchungaji au mtumishi fulani au mjane au mzee Fulani utaiotoa?

Mungu akikuambia SIKU ZOTE 30 ZA MWEZI FULANI hakuna kulala kitandani, ni kukesha utakubali?

UTAGUNDUA TUKO TAYARI KWA BARAKA ZA IBRAHIM LAKINI HATUKO TAYARI KUFANYA KAZI ZA IBRAHIM!

*KAMA KUNA KITU KWAKO AMBACHO BADO HUWEZI KUKITOA KWA MUNGU, BADO HUJAKUA KUTEMBEA KATIKA AGANO LA UTAJIRI ALILOLIISHI IBRAHIM BABA YETU!*

v) IBRAHIM ALIKUWA MTU WA KAZI/ ALIKUWA NA MIRADI NA BISHARA NYINGI NA SI MAOMBI NA KUTOA TU (MWANZO 13:2)!

-Ibrahim ALIKUWA MFUGAJI, tena tajiri sana wa mifugo! Wewe unafuga nini?

-Ibrahim ALIKUWA MTU WA KILIMO TENA CHA KISASA, alikuwa na VISIMA VYA UMWAGILIAJI ambavyo Isaka mwanae ALIVIFUKUA NA KUVITUMIA KUPANDA MBEGU KULE GERARI NA AKATAJIRIKA (Mwanzo 26:12-22)!

-Ibrahim ALIKUWA MTU WA MADINI
Alikuwa tajiri sana katika DHAHABU NA KATIKA FEDHA (SILVER).
Huyu ndugu alikuwa na migodi.
Huyu ndugu alikuwa dealer wa madini.
Sasa wewe mbona umekaa tu HUNA VYANZO VYA MAPATO TENA VINGI KAMA IBRAHIM?

unapaswa kuanza kuset biashara ndani ya miezi hii sita ijayo! Anzisha biashara hata kama ni ya kuuza maandazi, nyanya, wewe anza biashara au vyanzo kadhaa vya mapato, anza kufuga hata kuku au nguruwe au mbuzi ama mfugo wowote!
ACHA KUKAA TU NA AJIRA, UNASUBIRI MSHAHARA TU, UNAJICHELEWESHA!!!!!!

WEWE AMBAYE NI JOBLESS, UNAMZUIA MUNGU KUKUBARIKI.
Mungu hubariki “KAZI ZA MIKOO YETU” (Kumbukumbu 28:1-14) na si vinginevyo!

MUNGU HUJAZA GHALA NA KUFURIKISHA MASHINIKIZO KWA DIVAI MPYA (Mithali 3:9-10).
Maana yake ATAJAZA GHALA IPI WAKATI WEWE HUNA BIASHARA (MIRADI) HATA MITATU WALAU?

USIPOITENDEA KAZI HII KANUNI, UTAKUFA UNAKIRI NENO LAKINI HUTAONA BARAKA NA UTAJIRI KAMWE!

MAOMBI

OMBA KWA KADRI YA ULIVYOGUSWA NA KUELEWA SIRI HIZI ZA UFALME!

WEKA MAAZIMIO YA KUBADILI YALE AMBAYO HAUKUWA VIZURI!

MAFANIKIO NI KANUNI ASILIMIA 99% NA 1% MAOMBI.
NDIYO MAANA HATA WAPAGANI WANAOPATIA KANUNI WANA HELA NA UTAJIRI HUKU WALOKOLE WENGI WAOMBAJI WASIO NA KANUNI WAMEISHIA KUWA OMBAOMBA!

RUDIA SOMO HILI WALAU MARA 3 AU 4 NA KUANDIKA KILA AMBACHO ULIKUWA HUTENDI.

UKIKWAMA MAHALI, NJOO INBOX UULIZE.

HONGERA KWA SIKU HII YA SABA,
KAZANA UMALIZE ZOTE 10.
TUKUTANE KESHO SIKU YA NANE.

WEWE NI MBARIKIWA,
WEWE NI JIBU LA DUNIA YAKO.

Mchungaji kiongozi,
Makanisa ya ABC duniani,
Dickson Cornel Kabigumila.
28/07/2019.

 

HEKIMA ZA NDOA 4

“Ndoa ni taasisi ambayo unaungana na mtu mwingine ambaye ANAWEZA KUKUTIA MOTO kwenye KULIFUATA NA KULITIMIZA KUSUDI LA MUNGU… Wawili sahihi kila mmoja anakuwa CHUMA

Read More »

HEKIMA ZA NDOA 3

  “Kusudi la ndoa ni kujenga TIMU YA WANAOSADIANA NA KUINUANA. Wawili ni bora kuliko mmoja, MAANA MMOJA AKIANGUKA, MWENZIE ATAMUINUA. Ndoa sahihi ni muunganiko

Read More »